MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia Mbolea za Ruzuku na kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa haki.
Hayo amezungumza alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea amesema Rais amesikia kilio cha Watanzania na ametoa Ruzuku kwenye pembejeo za Kilimo.
“ Mh. Rais amemwaga Madini kwenye pembejeo za kilimo kutoka bei kubwa ya Mbolea kutoka zaidi ya laki moja na ishirini hadi hadi elfu Sabini”.
Thomas ametoa rai kwa Wakuu wa Wilaya kusimamia uandikishaji kwa kila Mkulima kwenye kijiji chake ili kila mtu apate pembejeo za ruzuku.
Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23,2022 ikiwa ni mpango wa Maendeleo wa miaka 10 ijaya.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Rais Samia ameamua kuleta pembejeo kwa Ruzuku ya Serikali kwa sababu anawajali sana wananchi wa Tanzania.
Amesema Serikali imetoa bilioni 50 na imebeba nusu ya bei na nusu atalipia Mkulima ili kuhakikisha Mwananchi anaondokana na tatizo la ukosefu wa Pembejeo.
Mhagama amesema Wakulima wasichukue mbolea hiyo na kuuza bali kila atakayechukua ahakikishe anatimiza malengo ya kilimo ili kuhakikisha Ruvuma inaendelea kuwa kinara kwa Chakula.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya MKuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 16,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.