Mkoa wa Ruvuma kuanzia Aprili 22 hadi 28 mwaka huu unatarajia kuanza kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 14.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko amesema katika kampeni hiyo wasichana 26,000 wanatarajiwa kuchanjwa chanjo hiyo.
“Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi HPV ni salama kabisa kwa kuwa imeanza kutolewa tangu mwaka 2018 na hadi sasa hakuna changamoto yoyote’’,alisisitiza Dr.Chomboko.
Dr.Chomboko amesema Mkoa wa Ruvuma pia unatarajia kutoa chanjo nyingine kwa Watoto walengwa 3,086 waliochini ya mwaka mmoja na kwamba huduma za chanjo zitatolewa nyumba kwa nyumba,vituo vya kutolea huduma za afya,shuleni na sokoni.
Kuanzia Aprili 22 hadi 28 mwaka huu,Mkoa wa Ruvuma unaungana na wadau wengine wa chanjo Duniani kutekeleza wiki ya chanjo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.