• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUVUMA yazalisha zaidi ya tani milioni mbili za mazao

Imewekwa kuanzia tarehe: November 1st, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mheshimiwa Kapenjama Ndile, amebainisha kuwa hadi kufikia mwezi Julai, 2024 Mkoa wa Ruvuma umezalisha tani  2,052,449 za mazao ya chakula.

Amesema hayo wakati akifungua kongamano la kilimo biashara lililofanyika katika ukumbi wa kanisa Katoliki Parokia ya Bombambili mjini Songea akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.

"Nchi imezalisha tani Milioni 8, Mkoa wa Ruvuma tumezalisha tani Milioni 2 unaweza kuona sisi sio wadogo tuna mchango mkubwa katika sekta ya kilimo" alisema Kapenjama Ndile.

Katika kongamano hilo Maafisa Ugani wamepatiwa Vishikwambi kwa ajili ya kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza tija katika kilimo, ambapo amewataka Maafisa hao kuvitumia vifaa hivyo vinavyotolewa na Wizara ya Kilimo vikiwemo Vishikwambi na pikipiki kwa matumizi sahihi na yaliyokusudiwa.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndg. Jumanne  mwankhoo ameliyataja lengo la kongamano ni kujiweka sawa kuelekea msimu wa kilimo 2024/25 ndio sababu ya wadau mbalimbali wa kilimo yakiwemo Makampuni ya wauzaji wa pembejeo na mbolea kujumuika.

Ameeleza kuwa kilimo biashara ni kilimo kinachotoa faida, hivyo amewasisitiza wakulima kuweka mipango ya kilimo mapema na kuacha kulima kwa mazoea.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Onesmo Ngao, ameishukuru Selous FM kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuandaa kongamano la kilimo biashara na kulitaja kama kielelezo na chachu kwa wakulima hususani kuelekea katika msimu mpya wa kilimo.

Kongamano la kilimo biashara kimefanyika mara ya pili mwaka huu ambapo mara ya kwanza lilifanyika  mwaka 2023 ikiwa ni sehemu ya juhudi za wadau wa kilimo kuboresha mbinu za uzalishaji na kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.