Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Riziki Suleiman Nkya amewaongoza akimama wa Mkoa wa Ruvuma kuadhimisha siku ya mama Duniani katika hafla aliyowaandalia akina mama wa Mkoa wa Ruvuma.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Chandamali mjini Songea alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma ndugu Rehema Sefu Madenge.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Bi. Riziki amewaasa akina mama kuzilea familia zao katika malezi bora kwa sababu wao ndiyo nguzo ya maendeleo ya familia.
Amewasisitiza akinamama hao kuishi katika maadili mema na kuwa mfano bora katika jamii inayowazunguka.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge akizungumza kwenye hafla hiyo amesema kuelekea katika siku ya familia Duniani ambayo kilele chake ni Mei 15 mwaka huu amewaasa akina mama kutumia siku hiyo kujitafakari kama wanatimiza wajibu wao kama akina mama katika familia.
Maadhimimisho ya siku ya kimataifa ya familia katika Mkoa wa Ruvuma yanatarajia kufanyika wilayani Namtumbo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.