Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema ni ndoto ya kila Taifa kuwa na wananchi wenye elimu bora itakayowawezesha kuingia kwenye soko la ushindani wa ajira katika kila sekta.
Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa tatu wa TAPSHA mkoa wa Ruvuma wa tathimini ya utekelezaji cha wa mtaala 2024 uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea (Songea Girls) iliyopo manispaa ya Songea.
"Ni ndoto ya kila Taifa kuwa na watu wenye afya njema, wenye elimu nzuri ambao wana fursa ya kuingia kwenye soko la ushindani wa ajira katika kila sekta, haya hayawezekani kama hatutawekeza kwa kiwango kikubwa katika elimu," alisema Kanali Ahmed.
Amesema serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, hivyo matarajio ya serikali na wazazi ni kuona matunda ya uwekezaji huo yanaleta faida chanya kwa taifa na mkoa.
Ameongeza kuwa ni wakati wa sekta zote za utendaji ndani ya mkoa kujitafakari kama zinafanya kazi inavyotakiwa, hasa sekta ya elimu kwa kuwa imekuwa ikifanya vibaya kitaifa.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Mwalimu Edith Mpinzile, akitoa taarifa ya elimu ya mkoa, amesema uchambuzi walioufanya umebaini kwamba tatizo kubwa la mkoa wa Ruvuma kufanya vibaya kitaaluma ni kukosa usimamizi wa ufundishaji, hivyo iwapo kila mmoja atawajibika katika eneo lake, mkoa utaweza kufanya vizuri kitaaluma.
Hata hivyo amesema wamefanya vikao vya kitaaluma ili kuwapitisha wataalamu katika changamoto za kielimu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo ambapo vikao hivyo vilihusisha maafisa elimu kata, wakuu wa shule za msingi na sekondari, na kikao cha wadau kilichojumuisha wataalamu wa elimu kutoka ngazi tofauti.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.