Mkoa wa Ruvuma umeshinda Tuzo ya Mkoa unaoongoza kuwa na mazao Mengi zaidi Tanzania yanayouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Akizungumza wakati anamkabidhi Tuzo hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma,Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma Peja Muhoja amesema Tuzo hiyo ya kitaifa imetolewa mjini Tabora kwenye maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani ambapo Tuzo mbalimbali zilitolewa
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo ofisini kwake mjini Songea,amewapongeza wakulima wa Mkoa wa Ruvuma ambao wamekubali kuuza mazao yako kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo amewashauri wakulima wengine katika maeneo mbalimbali kuhakikisha wanauza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ,mfumo ambao ameutaja kuwa na manufaa makubwa kwa wakulima ikiwemo kuuza mazao kwa bei kubwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.