MSHINDI wa kampeni ya NMB Bonge la mpango tumerudi tena wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amekabidhiwa zawadi yake ya pikipiki miguu mitatu a kwenye hafla iliyofanyika mjini Mbinga.
Mkoa wa Ruvuma umetoa washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu ambazo NMB kwa nchi nzima imetoa pikipiki 50.
Mshindi wa Mbinga ni Aikamesia kuro na mshindi wa Songea Ahmed Dani.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni rasmi Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amesema Kanda ya Kusini ina matawi 20 ya NMB liliwemo tawi la Mbinga.
Amesema NMB ilizindua kampeni ya NMB Bonge la mpango mwaka jana lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi kufungua akaunti na kujiwekea akiba zao wenyewe.
“Wataalam wanashauri kipato chochote unachokipata ni vema kutenga kwenye makundi matatu,kiasi kuweke akiba ambayo itakusaidia kesho,kiasi cha pesa kutenga kwenye matumizi yako na kiasi kuwekeza kwenye shughuli inayoifanya ili iwe endelevu’’,alisisitiza Shango.
Amesema NMB inatoa elimu ya wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba ambapo hivi sasa watalaam wa NMB wanapita katika shule za msingi na sekondari kutoa elimu hiyo ili kuwawezesha watoto hao kuwa na tabia ya kuweka akiba,matumizi na kuwekeza tangu wakiwa wadogo.
Meneja huyo wa Kanda NMB ameitaja Benki hiyo kuwa ina akaunti mbalimbali ambazo zitamsaidia mteja kuweka akiba na kutumia vizuri pesa zake kulingana na anachokipata.
Shango amesema Oktoba 2022 NMB ilizindua kampeni ya NMB Bonge la mpango kuhamasisha wateja kuweka akiba walau kuanzia shilingi 100,000 hivyo kuingia moja kwa moja kwenye droo.
Hata hivyo amesema wananchi wengi waliingia kwenye droo hiyo ambapo NMB ilikuwa inashindanisha Zaidi ya shilingi milioni 300 na kushindanisha pikipiki za miguu mitatu 50 na kwamba kwenue droo hiyo NMB ilikuwa inatoa shilingi 200,000 kila wiki.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Tawi la Mbinga Enhard Tambo amewahamasisha wananchi wa Mbinga kuendelea kufungua akaunti NMB kupitia mawakala Zaidi ya 100 waliopo maeneo mbalimbali katika wilaya ya Mbinga ili kuingia kwenye droo ya kampeni ya Bonge la mpango.
Amesema kampeni hiyo inamwezesha mtu yeyote kushinda awe mkulima,mfanyakazi au mjasirimali na kwamba mshindi wa Mbinga alikuwa anafanya miamala ya kawaida.
Kwa upande wake mshindi wa pikipiki hiyo Aikamesia Kuro ameishukuru Benki ya NMB kwa kumpatia zawadi hiyo ambayo amesema itamsaidia katika katika biashara yake duka la spea ambapo sasa ataweza kuwapelekea wateja wake mizigo hadi nyumbani kwao.
NMB ni Benki salama,kwa miaka tisa mfululizo imeendelea kuongoza kwa ubora nchini Tanzania.
Imeandikwa na Albano Midelo,Ruvuma
Machi 10,2022
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.