WAKALA wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,imetiliana saini na wakandarasi mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya Sh.bilioni 5,473,744,522.32.
Miradi hiyo inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 70.2 hadi kufikia asilimia 85 kwa wananchi waishio vijijini ifikapo mwaka 2025
Meneja wa RUWASA wilaya ya Tunduru Maua Mgallah,ameitaja miradi hiyo ni mradi wa maji Misechela-Liwanga wenye thamani ya Sh.bilioni 3,020,150,910.00,mradi wa maji Tuwemacho wenye thamani ya Sh.bilioni 1,054,232,603.55 mradi wa maji Msinji utakaotekelezwa kwa Sh.bilioni 1,069,014,450.00 na mradi wa Hulia uliotengewa Sh. Sh.bilioni 1,206,605,519.28
Aidha alisema,RUWASA inatarajia kutekeleza miradi miwili ya Namwinyu-Namakunga wenye thamani ya Sh.milioni 450,000,000 na mradi wa Nakapanya-Namakambale kwa gharama ya Sh. 150,000,000 hivyo kufanya miradi itakayotekelezwa kwa mwaka 2023/2024 kufikia 9 kwa gharama ya Sh.bilioni zaidi ya bilioni sita.
Alisema,kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa watu 43,625 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 12.6 ya wakazi wa vijijini,hivyo kufikia asilimia 82.6. ya utoaji wa huduma ya maji.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro alisema,lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanaoishi vijijini nao wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 85 na kuwapunguzia kama siyo kumaliza kabisa changamoto ya kwenda umbali mrefukutafuta huduma ya maji.
Mtatiro,ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika vijiji mbalimbali wilayani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.