• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUWASA kutumia bilioni 600 kusambaza maji vijiji

Imewekwa kuanzia tarehe: November 22nd, 2022

MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo amesema RUWASA inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 600 kusambaza maji vijijini.

Amesema hayo baada ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Lipaya Halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na  RUWASA.

Amesema kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi ya maji, Benki ya Dunia imeridhia kuongeza fedha  Dola  milioni 300 za Marekani  ambazo ni sawa na  zaidi ya shilingi bilioni 600 zote zinakwenda kuboresha maji vijijini.

Ameahidi mradi wa maji Lipaya unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja unatarajia kuanza kutoa maji kabla ya Desemba 30 mwaka huu ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

“Shida ya maji kwa utamaduni wa Afrika wanaumia zaidi ni akinamama kwa sababu wao ndiyo wanakwenda kutafuta maji,sisi kwetu RUWASA uwepo wa Rais Mama umesababisha bajeti ya fedha  kuwa kubwa hivyo kuweza kutekeleza miradi mingi ya maji ndani ya muda mfupi’’,alisisitiza Mhandisi Kivegalo.

Amempongeza  Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga kwa kusimamia na kutekeleza vizuri miradi ya maji hali iliyosababisha kuongezewa bajeti ya miradi ya katika Mkoa wa Ruvuma toka bilioni saba hadi kufikia  bilioni 11.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama amewapongeza RUWASA kwa juhudi wanazofanya za kuhakikisha wanamaliza kero ya maji maeneo ya vijijini likiwemo Jimbo la Peramiho.

Amesema katika historia ya Jimbo la Peramiho hii ni mara ya kwanza kwa timu nzima kutoka RUWASA makao makuu kufika kukagua  utekelezaji wa miradi ya maji  na ile yenye changamoto kuitafutia ufumbuzi ili wananchi wapate maji safi.

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA akiwa na watendaji wakuu toka makao makuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maji na miradi yenye changamoto kuipatia ufumbuzi ili wananchi waanze kunufaika na upatikanaji wa maji safi na salama.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Pololet Mgema amesema Mkoa wa Ruvuma una kila sababu ya kumshukuru Rais kwa kuupiga  mwingi kutokana na kutoa fedha za kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji.

“Kuna watu  wakisikia wananchi na viongozi wanamshukuru na kumsifia Rais wetu kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa watanzania wanakasirika,sisi tunaotambua kazi yake tunasema anaupiga mwingi’’,alisema.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 22,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.