• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUWASA Ruvuma kukamilisha miradi 19 ya maji

Imewekwa kuanzia tarehe: April 12th, 2021

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Ruvuma imedhamiria kukamilisha miradi ya maji 19 ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Rebman Ganshonga, amesema miradi hiyo ikikamilika asilimia 72 ya wananchi takribani milion 1.5 waishio vijijini watapata maji safi na salama.

Ilani ya Chama Tawala CCM inaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 asimilia 85 ya wakazi wa maeneo ya vijijini na asilimia 95 kwa mijini wawe wanapata huduma ya maji safi na salama.Ili kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa Meneja RUWASA Mkoa wa Ruvuma amesema hivi sasa wanatekeleza miradi mbalimbali ilioanishwa kwenye bajeti ya mwaka 2020/2021.

Hata hivyo amesema kuna miradi mitano iliyochukua muda mrefu kukamilika katika Mkoa wa Ruvuma,hata hivyo amesema tangu RUWASA kuanzishwa miradi mitatu miongoni mwa hiyo imekamilika.Ganshonga ameitaja miradi hiyo iliyokamilika kuwa ni Likuyusekamaganga, Mkongo na Matemanga na kwamba  hivi sasa inatoa huduma kwa wananchi na kwamba miradi miwili iliyobaki anasema ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

“Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na jumla ya miradi sita yenye changamoto, lakini tangu RUWASA ianze kazi miradi mitano imekamilika na mmoja uliobaki upo kwenye hatua za mwisho za utekelezaji’’,alisisitiza.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma amesema Katika mwaka wa fedha utakaoanzia Julai mwaka huu wanatarajia  kutekeleza zaidi ya miradi 28 kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 12 na kwamba watatumia mito na visima katika kutekeleza miradi hiyo kama mikakati ya muda mfupi.

Kuhusu mikakati ya muda mrefu Ganshonga amesema Wizara ya Maji inatarajia kujenga mradi mkubwa ambao utatumia maji ya Ziwa Nyasa na utahudumia maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani ya Lindi na Mtwara ambayo pia inakabiliwa na changamoto.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme anaipongeza serikali kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni saba kwa ajili ya kuboresha miundombinu na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa miji ya Songea, Mbinga na Tunduru.Amesema kupitia RUWASA na SOUWASA, kazi kubwa imefanyika ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni tano kati ya bilioni saba kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya maji ndani ya mkoa wa Ruvuma.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma




Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.