RUWASA Songea yatoa mafunzo na vyeti kwa jumuiya tisa za watumia maji
WAKALA wa maji vijijini RUWASA wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imetoa mafunzo na kugawa vyeti kwa jumuiya tisa za watuamia maji katika Halmashauri za Madaba na Halmashauri ya Songea.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Songea Klub Mtaalam wa RUWASA Wilaya ya Songea Samweli Sanya amesema Ruwasa kwa kushirikiana na jumuiya hizo zilizoundwa watahakikisha wananchi wanapata huduma ya maji endelevu kwa usimamizi na uendeshaji na wananchi watachangia huduma hiyo.
Mgeni rasimi katika mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro amesema lengo la RUWASA ni kutekeleza na kuiwezesha jamii kuwa na jumuiya ya maji imara na kuleta tija endelevu kwa wananchi vijijini.
Amesema Jumuiya waliopata mafunzo hayo wawe walimu na wasimamizi wazuri katika kutunza miundo mbinu iliyopo katika jumuiya za watumia maji ili wananchi wapate huduma bora na endelevu.
‘’Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunda wakala wa maji safi na mazingira vijijini RUWASA inatusaidia kuleta huduma nzuri karibu na wananchi wa vijijini’’,alisema.
Ndumbaro amesisistiza kuwa Jumuiya tisa zilizopata mafunzo hao zihakikishe wananchi wanapata huduma nzuri ya maji na watunze mazingira,Serikali imetoa fedha nyingi katika miradi mikubwa ya maji ambapo amewaasa wananchi kutunza vyanzo vya maji na kuacha kukata miti hovyo.
‘’Nitolee mfano mzuri katika milima ya Lihanji wilayani Songea kuna vyanzo vya maji na vyanzo vyake vinalisha maeneo makubwa katika tarafa ya Ruvuma Peramiho na Kilagano vinatumia kutoka milima ya Lihanji’’,alisisitiza.
Amesema licha ya mafunzo waliyopata kuna rasimu ambazo zimetolewa na kupitishwa Jumuiya zote ambazo ameagiza wakasimamie na kwamba miundombinu inapoharibika irekebishwe kwa kutumia michango wanayochangisha kwa wananchi.
RUWASA imeanzisha kupitia sheria namba tano iliyopitishwa na Bunge mwaka 2019 na kuanza kutumika Julai mosi 2019.
Imeandikwa na Anet Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Agosti 3,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.