Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura ametoa tuzo kwa shule za Sekondari zilizofanya vizuri katika Mtihani wa kidato cha nne na kidato cha pili mwaka 2024 pamoja na kukabidhi kilo 380 za sukari kwa shule za Sekondari za Serikali 38 ikiwa ni motisha kwa walimu katika ujifunzaji na ufundishaji.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla ya utoaji wa tuzo za taaluma kwa shule za Sekondari zilizofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha pili na Kidato cha nne mwaka 2024.
Pamoja na tuzo hizo Mkurugenzi amewataka walimu hao kutimiza majuku yao ya ufundishaji ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata umahiri na weledi.
“ Tuzo hizi ni motisha katika kuboresha Elimu katika Halmashauri yetu sisi ambao hatujapata tujitahidi tupambane na wale ambao leo mmepata ongezeni spidi” Amesem
Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Rashid Bundalah ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 3,522 ikiwa 1,368 wavulana na 2,154 wasichana kutoka katika shule 49 walifanya Mtihani wa Upimaji Kitaifa Kidato cha pili mwezi Novemba 2024.
Aidha watahiniwa wapatao 2,205 ikiwa 893 wavulana na 1,312 wasichana kutoka katika shule 46 walifanya Mtihani wa Taifa Kidato cha nne mwezi Novemba 2024.
Ili kuinua ufaulu na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi Bundalah amethibitisha kuendelea kufuatilia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji na kuchukua hatua stahiki kwa walimu wasiotimiza majukumu yao pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaosababisha wanafunzi kukatisha maaasomo.
Kwa upande wake mwalimu Athanas Mbele Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ameeleza tukio hilo ni deni kwao katika kuhakikisha wanainua ufaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.