Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu stephen Ndaki imeanza ukaguzi wa miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa sekondari ya wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan unaotekelezwa katika eneo la Migelegele Kata ya Rwinga ambapo serikali imetenga shilingi bilioni nne kutekeleza mradi huo.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma,Mkuu wa shule Mwl Amos Mapunda amesema hadi sasa zimetumika shilingi bilioni tatu kujenga madarasa 12,maabara nne na ,jengo moja la Utawala .
Majengo mengine ambayo yanaendelea kujengwa ni nyumba za walimu,mabweni matano,vyoo matundu 16,bwalo na ,mfumo wa maji safi .
Mkuu wa shule ametoa rai kwa serikali kumalizia kiasi cha shilingi bilioni moja iliyobakia ili kukamilisha ujenzi huo
Sekondari hiyo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano Julai 2023 na kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza Desemba 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.