Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Philimon Magesa amesema utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa sekondari maalum ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliyopo eneo la Migelegele wilayani Namtumbo umefikia zaidi ya asilimia 95.
Amesema kazi nyingi zimekamilika na kilichobakia hivi sasa ni umaliziaji ambapo hadi mwishoni mwa mwezi Agosti utekelezaji unatarajia kufikia asilimia 100.
Serikali ya Awamu ya Sita hadi sasa imetoa zaidi ya shilingi bilioni 4.3 kutekeleza mradi wa shule hiyo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.