Serikali ya Awamu ya Sita imekamilisha ujenzi wa sekondari ya mfano ya wasichana katika Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwa gharama ya shilingi bilioni 4.35. Shule hiyo, iliyosajiliwa kwa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan, ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200 kutoka kidato cha kwanza hadi cha sita.
Hadi kufikia Januari 31, 2025, shule hiyo inatarajiwa kuwa na wanafunzi 700, huku ikiwa na miundombinu ya kisasa inayofaa kwa malezi na elimu bora ya wasichana.
Shule hiyo ilizinduliwa rasmi Septemba 2024 na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma.
Huu ni moja ya sekondari 26 za bweni kwa wasichana zilizojengwa nchini kwa gharama ya shilingi bilioni 106.6.
Mradi huu unalenga kuboresha elimu ya wasichana na kutoa fursa sawa kwa elimu nchini Tanzania.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.