Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkoa wa Ruvuma, wamefanya ziara ya Kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, ikiwemo ujenzi na ukamilishwaji wa vyumba vya maabara, sambamba na ujenzi wa zahanati kwa baadhi ya kata.
Wataalamu hao waliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri hiyo wakitokea idara ya Elimu Sekondari, Afya, Mipango , Maendeleo ya Jamii pamoja na Manunuzi ambapo walitembelea Ujenzi na Umaliziaji wa Vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari kilimani kati ilioko kata ya kilimani, Shule ya Sekondari Luhuwiko pamoja na Shule ya Sekondari Lusonga.
Hata hivyo wataalamu hao waliweza kutembelea na kukagua Miradi ya Ujenzi wa zahanati Mahande katika kata Utili huku ujenzi huo ukitumia mapato ya ndani sambamba na nguvu za wananchi.
Aidha walitembelea Ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Myangayanga pamoja na Kituo cha Afya Mbangamao katika kata ya Mbangamao, huku ujenzi wa vituo hivyo ukipata fedha kutoka Serikali kuu.
Wataalam hao kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameridhia namna ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa namna ya ufanisi na ubora, sambamba na kutoa maelekezo katika baadhi ya miradi kwa mapungufu waliyoyabaini huku wakiagiza kuyafanyia marekebisho kabla ya miradi hiyo kukamilika.
Miradi iliyo tembelewa imeghalimu zaidi ya kiasi cha fedha Bilioni 1.4 kutoka Serikali kuu na zingine kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri katika kukamilisha ujenzi na Ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika baadhi ya kata Halmshauri ya Mji wa Mbinga .
Wananchi wameendelea kumpongeza Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Mbinga katika Sekta ya Afya, Miundombinu ya Elimu, Maji na Barabara, kuwa imekuwa chachu kwao katika kuleta maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.