• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SEKTA ya madini Ruvuma yang’ara

Imewekwa kuanzia tarehe: May 22nd, 2025

Katika kipindi kisichozidi miezi kumi, Mkoa wa Ruvuma umeandika historia mpya kwenye sekta ya madini baada ya kufanikisha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kufikia Shilingi Bilioni 32.5.

Hii ni kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 ulioanza Julai 2024, na makusanyo hayo ni hadi kufikia tarehe 19 Mei 2025, kiasi ambacho ni karibu na lengo la Shilingi Bilioni 33.15 walilopangiwa na Serikali.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi, alieleza mafanikio haya mbele ya wanahabari wa Tume ya Madini, akibainisha kuwa matarajio ni Mkoa huo kuvuka lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 100 kabla ya kufika mwisho wa mwaka wa fedha mwezi Juni.

Mafanikio haya yanaashiria nidhamu ya ukusanyaji mapato, usimamizi madhubuti, na uwekezaji ulioimarika katika sekta ya madini.

Mhandisi Bikulamchi alitaja biashara ya makaa ya mawe kuwa kichocheo kikuu cha mafanikio hayo, akieleza kuwa makaa ya Ruvuma yamebainika kuwa bora zaidi kitaifa na kimataifa.

Makaa hayo sasa yanauzwa kwa wingi katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda pamoja na masoko ya Bara la Asia na Ulaya, jambo linaloongeza thamani ya madini ya mkoa huo.

Mbali na makaa ya mawe, Ruvuma pia imejaaliwa kuwa na aina nyingi za madini ikiwemo dhahabu, shaba, chuma, urani, madini ya ujenzi na vito.

Wingi na utofauti wa madini haya vimeifanya sekta hii kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa Serikali na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma, huku fursa mpya za kiuchumi zikiendelea kufunguka kila uchao.

Katika kuhakikisha biashara ya madini inakuwa shirikishi na yenye manufaa kwa pande zote, Serikali kupitia Tume ya Madini imeanzisha masoko rasmi mawili ya madini – Soko la Madini Songea na Soko la Madini Tunduru.

Masoko haya yameongeza uwazi, usalama na usawa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, na kuwezesha Serikali kukusanya mapato kwa njia halali na sahihi.

Mhandisi Bikulamchi aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini, ikiwemo usambazaji wa teknolojia migodini, huduma za chakula, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini.

Ruvuma sasa siyo tu mkoa wa kilimo, bali pia miongoni mwa nguzo kuu za maendeleo ya sekta ya madini nchini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MSIKIMBILIE hasara,serikali inakuja na bei ya neema kwa mahindi Julai

    May 31, 2025
  • WAKULIMA Namtumbo wachuma neema ya ufuta kwa teknlojia mpya ya mnada wa kidigitali

    May 31, 2025
  • RUSHWA yazidi kuporomoka na kukosa nafasi Ruvuma

    May 31, 2025
  • SERIKALI yatoa fidia ya bilioni 2.5 kupisha mradi wa umeme wa Grid Songea-Tunduru

    May 31, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.