VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Ruvuma wametakiwa kuyasema mazuri yote yanayofanywa na Rais, Wabunge na Madiwani ili wananchi waelewe kwa uwazi mambo hayo ambayo kimsingi yameainishwa kwenye ilani ya Ccm ya mwaka 2020/ 2025
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Songea Mjini wa kupokea Utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Kipindi Cha Miaka mitano tangu 2018 - 2023 ya Uongozi wa Dkt.Damas Ndumbaro Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri Wa Katiba na Sheria, Ulioifanya Songea Mjini.
Mwisho alisema kuwa yapo ambayo yamefanyika na yanaonekana kwenye sekta mbalimbali lakini viongozi wa Ccm kwenye maeneo yenu hamyatangazi, hali ambayo inapelekea kuzuka kwa masikitiko kwa wananchi
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Ndumbaro ameyaeleza mafanikio aliyoyapata kwa miaka mitano toka 2018-2023 na ameyaandika kwenye kitabu chenye kurasa 140, myasome na myaeleze waziwazi ili wanachama na wananchi wayaelewe namna Mbunge anavyohangaika kuwaletea maendeleo
“Nakupongeza sana Mbunge Dkt Ndumbaro kwa kazi kubwa unayoifanya katika Jimbo lako na Nchi kwa ujumla, sie kama chama ndio tulikukabidhi Ilani ili uitekeleza hakika umefanya makubwa kwa muda mfupi, hongera sana na tutaendelea kuyasema haya kila mara ili kukirahisishia chama katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na vijiji mwaka 2024 na uchaguzi mkuuu mwaka 2020” alisema Mwisho
Akisoma ilani hiyo ya miaka mitano Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba alisema kuwa mambo mengi yametekelezwa katika sekta zote na kuwafanya wananchi waendelee kufurahia uwepo wa Viongozi wanaotokana na Ccm
Dkt Ndumbaro alisema katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2023 Serikali imetekeleza na kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo na ujenzi wa vyumba vya madarasa fedha za UVIKO 19, ujenzi wa vituo vya afya vipya vitano 5 na Hospitali ya Wilaya 1 pamoja na Hosptali ya Rufaa ya Mkoa 1 iliyopo Mwengemshindo,
“Kujengwa Chuo kikuu kipya cha Uhasibu Arusha, Masoko mawili ya kisasa (Manzese), ujenzi wa uwanja wa ndege, daraja ya Matarawe- Mjiwema, Mikopo kwa vikundi bil. 1 kwa mwaka, Barabara kutoka Sanga one hadi Tanroad, kujenga barabara ya kiwango cha Lami km 13 katika kata ya Mfaranyaki, Misufini, na Majengo na miradi mingineyo kutawafanya wananchi kupiga hatua ya kimaendeleo” alisema Dkt Ndumbaro.
Alisema pamoja na ukarabati wa miundombinu chakavu ya madarasa, barabara za mitaa, maji kwa baadhi ya kata, uhitaji wa vituo vya afya katika kata ya Bombambili, Ruhuwiko, na Lizaboni, uhitaji wa shule za Sekondari mpya kwa kata ambazo hazina Sekondari za kata kama Seedfarm, Ruhuwiko na Ndilima Litembo.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema Manispaa imetenga bajeti ya shilingi Mil. 20 kupeleka kila kata ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kata husika ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya madarasa chakavu.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt, Frederick Sagamiko alisema changamoto ya barabara za mitaa haita kuwepo kwa sasa kwani Manispaa imeandaa utaratibu kupitia TARURA wa kutatua chanagamoto hizo ambapo ameagiza kata zote 21 kuleta taarifa zenye ufafanuzi maalum wa mahitaji ya miundombinu korofi ambayo inahitaji kutekelezwa ikiwemo na barabara za mitaa, vivuko vyote, madaraja, na mifereji ili TARURA waweze kutekeleza .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Songea Mjini Mwinyi Msolomi amewataka Viongozi mbalimbali kuacha Mipasuko ambayo itapelekea kuzorotesha shughuli za kimaendeleo.
Msolomi alisema lengo kuu la Serikali katika kuaajiri wataalamu ni kwa ajili ya kusimamia na kuratibu shughuli shughuli zote za Serikali pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi,
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego alisema kuwa Wananchi wa Songea wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kutoa fedha nyingi ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbalimbali
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.