Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametoa rai kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa kupiga namba za simu walizopewa ili waweze kuhesabiwa.
Kanali Thomas ametoa rai hiyo kwenye kikao cha tathmini ya wajumbe wa sensa ngazi ya Mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mipango mjini Songea.
Kwa upande wake Mratibu wa sensa Mkoa wa Ruvuma Mwamtum Athuman Uhenga amesema kazi ya kuhesabu sensa katika kaya mkoani Ruvuma imefikia hatua nzuri hadi kufikia Agosti 30 mwaka huu. “Kazi inayoendelea kwa sasa ni ukusanyaji wa taarifa za majengo yote yaliyomo katika Mkoa,makarani wote wapo kazini kuhakikisha majengo yote yanajaziwa taarifa zake”,alisema Uhenga.
Hata hivyo amesema kaya zilizobaki za mtu mmoja mmoja ambazo hazijahesabiwa zimeendelea kupiga simu ili zihesabiwe.Amelitaja jukumu la kuwahesabu mtu mmoja mmoja linafanywa na timu ya wakufunzi ambao walikuwa ni wasimamizi kwenye zoezi la sensa.
Amesema Mkoa umepata mafanikio makubwa kwenye zoezi la sensa kutokana na makarani kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Serikali za mitaa na vitongoji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.