Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe. Kisare Makori amesema serikali haitakuwa tayari kuona maslahi yanayohusiana na wakulima yanachezewa kwa namna yoyote ile.
Mhe. Makori amesema hayo kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya Vyama vya Ushirika katika wilaya yake kupora haki za wakulima.
Amesema kati ya malalamiko anayopelekewa ofisini kwake, masuala yanayohusiana na vyama vya ushirika yanashika namba moja huku akisema kilio cha wakulima ni ukomo wa madeni na malipo ya awamu ya pili.
Mheshimiwa Makori amesema hayo wakati wa mkutano na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga chini ya Mwenyekiti wa CCM-Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho.
Makori amesema kuwa tayari amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Wilaya ya Mbinga wawaandikie maafisa ushirika na viongozi wote wa vyama ushirika nini cha kufanya kuhusu ukomo wa madeni na malipo ya wakulima.
“Nimewataka wawaandikie kuwa hakutakuwa na uidhinishwaji wa ukomo wa madeni na hakutakuwa na malipo ya wakulima kwenye vyama vya msingi bila taarifa kufika ofisi ya mkurugenzi,” alisema.
Kwa mujibu wa Mhe. Makori, kati ya vyama vya ushirika 120 vilivyopo katika mkoa wa Ruvuma, vyama 100 vipo wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.