• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI ilivyoboresha barabara Mbinga na Mbambabay

Imewekwa kuanzia tarehe: June 4th, 2024

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeboresha barabara kwa kiwango cha lami katika Wilaya za Mbinga na Nyasa hivyo kuleta unadhifu na mvuto katika miji hiyo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mhandisi Silvester Chinengo wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa barabara wilayani Mbinga,Mhandisi Chinengo amesema TARURA ilitengewa kiasi cha shilingi milioni 500 kujenga barabara ya lami nyepesi yenye urefu wa kilometa 0.75,

Amesema ujenzi wa barabara hiyo ulianza Septemba 14,2023 na ulitarajiwa kukamilika Mei 28,2024 ambapo hadi sasa utekelezaji wa mradi huo ni Zaidi ya asilimia 95.

“Mradi huu ni utekelezaji wa mpango wa kujenga barabara za Daniel na Mjimwema wilayani Mbinga,zenye jumla ya kilometa 3.6 mwaka 2022/2023,awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa  barabara ya Mjimwema  kilometa 1.2 na barabara ya Daniel yenye urefu wa kilometa 2.2 kwa gharama ya shilingi bilioni moja’’,alisema Mhandisi Chinengo.

Hata hivyo amesema  awamu ya pili ya ujenzi imehusisha ujenzi wa kilometa 0.9 kwa gharama ya shilingi milioni 500 ,mradi ambao umetekelezwa  katika mwaka 2023/2024.

Amesema TARURA inatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa kilometa 0.5 zilizosalia kwa gharama ya shilingi milioni 500 katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Nyasa Mhandisi Thomas Kitusi akizungumzia utekelezaji ujenzi wa barabara kiwango cha lami katika Mji wa Mbambabay amesema wilaya hiyo inatekeleza mradi mmoja wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 0.8.

Amesema mradi huo umetengewa shilingi milioni 500 katika bajeti ya mwaka 2023/2024 ambapo hadi sasa mradi umefikia asilimia 99 na kwamba kazi zilizosalia amezitaja kuwa ni  kufunga taa tano za kumulika barabarani na kazi ya kuchimba mashimo ya kuweka nguzo.

Ametaja manufaa ya mradi huo kuwa ni kuongeza mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 4.68 zilizokuwepo katika mwaka 2022/2023 hadi kufikia kilometa 5.48,kupunguza  gharama za matengenezo na kuleta unadhifu na madhari ya mji.

TARURA Mkoa wa Ruvuma una mtandao wa barabara zenye jumla ya kilometa 7146.21 zilizosajiriwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.