• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI ilivyodhamiria kurejesha mafuvu 200 ya mashujaa likiwemo fuvu la Nduna Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 23rd, 2020

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje imedhamiria kuyarejesha nchini mafuvu 200 ya mashujaa yaliyohifadhiwa nchini Ujerumani.

Mafuvu hayo likiwemo fuvu la Jemedari wa kabila la wangoni Nduna Songea Mbano yalichukuliwa na wajerumani mwaka 1906 kutokana na mashujaa hao kuonesha upinzani mkubwa dhidi ya utawala wa wakoloni katika vita ya Majimaji iliyopiganwa kati ya mwaka 1905 hadi 1907.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki anasema mafuvu hayo yakirejeshwa nchini ,yatafanyiwa maziko ya heshima yanayostahili kwa mashujaa.

Anasema kwa miaka mingi kumekuwa na mjadala unaohusu urithi wa nchi yetu uliochukuliwa na kuhifadhiwa nje ya nchi yakiwemo mafuvu ya mashujaa wa vita ya Majimaji yaliopo Ujerumani kurejeshwa nchini.

Hata hivyo anasema,Wizara imebaini baadhi ya mafuvu ya mashujaa hao yalitoka Songea na kwamba Wizara  inaahidi kushirikiana na jamii zote za kitanzania zenye kudai urithi huo kurejeshwa nchini kwa kuainisha aina za urithi unaopaswa kurejeshwa nchini.

“Madai  ya urithi huo yatawasilishwa rasmi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,ndugu zetu wangoni,tunahitaji kurejesha heshima kwao kwa sababu wao walitupa heshima kubwa ya kulinda,nchi yetu,mila na desturi zetu’’,anasema Dkt Nzuki.

Anaitaja aina moja muhimu ya kurejesha heshima  kwa wangoni ni kurejesha mafuvu ya mashujaa hao ili yaweze kupatiwa maziko ya heshima na kwamba  Wizara ya Maliasili na Utalii ipo tayari kuhakikisha mafuvu hayo yanarejea nchini.

Akizungumzia umuhimu wa kuwakumbuka mashujaa katika harakati za ukombozi,Dkt.Nzuki anasisitiza watanzania kutambua na kujifunza utamaduni wa jamii ya wangoni hasa namna mababu zetu walivyojitoa muhanga kupinga uonevu wa kikoloni wa kijerumani na kuamua kupigana nao.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Septemba 23,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.