• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI ilivyomaliza kero ya maji Kitanda Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: September 12th, 2023

SERIKALI YAMALIZA KERO YA MAJI KWA WANANCHI WA KITANDA MBINGA
MKAKATI wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa kumtua mama ndoo kichwani umetekelezwa kwa vitendo kwa wakazi wa kijiji cha Kitanda Halmashauri ya mji Mbinga mkoani Ruvuma.
Hatua hiyo imetokana na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA)wilayani Mbinga,kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji utakaohudumia  zaidi ya wakazi 3,600 wa kijiji hicho na kijiji cha Mangwangala.
Wakizungumza jana wananchi wa kijiji hicho wamesema,kukamilika kwa mradi huo kumewaondolea changamoto ya kutafuta  huduma ya maji umbali mrefu kiasi cha kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo na kuongeza kuwa,hiyo ni mara ya kwanza kushuhudia maji ya bomba yakitoka kwenye kijiji hicho.
Daud Mapunda alisema,baada ya kukamilika kwa mradi huo maisha yao  yatakuwa mazuri na kuimarika kwa ndoa nyingi ambazo ziliyumba kutokana na kero ya maji ambapo akina mama walitumia muda mwingi kwenda kutafuta huduma hiyo badala ya kuhudumia ndoa zao.

Athanas Mbunda mkazi wa kijiji cha Kitanda alisema,katika maisha yao yote wamekuwa na changamoto ya maji safi na salama kwa muda muda mrefu na kuna wakati walilazimika kutafuta maji mbali na kijiji chao.

Alisema,katika kutafuta huduma ya maji kuna wakati mwingine walilazimika kulala mtoni na kurudi siku ya pili yake na hivyo kusababisha migogoro kwa baadhi ya familia.

“mimi nina umri wa zaidi ya miaka 45,na katika umri wangu huu sijawahi kuona maji ya bomba hapa kijijini kwetu,tunaishukuru serikali yetu kwa kutambua changamoto  tuliyonayo na leo tumeona mradi wa maji uliotekelezwa na ndugu zetu wa Ruwasa”alisema.

Diwani wa kata ya Kitanda Aureus Ngonyani,ameishukuru Ruwasa kukamilisha mradi na serikali kutoa fedha ambazo zimemaliza kero ya huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Kitanda na Magwangala.

Aidha,ameiomba serikali kupitia RUWASA kufikisha huduma ya maji kwenye vijiji vitatu vilivyobaki ambavyo bado wananchi wake wanaendelea kuteseka kwa kukosa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Mbinga Mhandisi Mashaka Sinkala alisema,mradi ulianza utekelezwa mwezi Julai 2022 kwa kutumia mkandarasi M/S JB Mwalongo kwa gharama ya Sh.milioni 473,101,856.40.

Hata hivyo alisema, muda wa utekelezaji wake ulisogezwa mbele kwa miezi minne  zaidi kutokana na changamoto ya mvua na taratibu za msamaha wa kodi kuchelewa.

Alisema,mradi huo umekamilika tangu mwezi Juni 2023 kwa asilimia 100 na sasa uko kwenye muda wa matazamio ya mwaka mmoja na mkandarasi amelipwa Sh.milioni 257,555,604.00 ambazo ni sawa na asilimia 54.4 na  unatoa huduma kwa wananchi.

Ametaja kazi zilizofanyika ni kujenga tenki moja la lita 150,000,kuchimba mitaro na kulaza mabomba umbali wa kilomita 19,935  ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji na ujenzi wa chanzo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.