• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI imefanya juhudi kubwa za kuleta magari ya wagonjwa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: October 3rd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema serikali imefanyya juhudi kubwa za kuleta magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) ili kuimarisha huduma za rufaa za wagonjwa hasa mama na mtoto.

Kanali Abbas amesema hayo wakati anazungumza katika  makabidhiano ya mwendelezo wa mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa akina mama wajawazito (M-mama) kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Amesema hivi sasa Mkoa wa Ruvuma una jumla ya magari ya kubeba wagonjwa 21 kati ya hayo magari 15 ni mapya kabisa.

“Natambua kuwa kiuhalisia magari ya kubebea wagonjwa yaliyopo hayawezi kutosheleza mahitaji ya kusafirishia rufaa kutoka pande zote za Mkoa  wetu kutokana na sababu mbalimbali,hivyo pengo hili litaendelea kuzibwa kwa kuwatumia madereva ngazi ya jamii ambao wamesaini mikataba katika Halmashauri zetu’’,alisisitiza Kanali Abbas.

Amesema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto lengo likiwa ni kupunguza  na kumaliza tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya Watoto wachanga vinavyozuilika.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote mkoani Ruvuma kusimamia mfumo wa M-mama kwa kuhakikisha magari ya wagonjwa  yanakuwa  tayari wakati wote na kuhakikisha kunakuwa na utaratibu mzuri wa madereva ngazi ya jamii na kusimamia kuharakisha malipo yao kulingana na mikataba.

Kanali Abbas amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Halmashauri zimetenga bajeti zitakazowezesha utekelezaji wa shughuli za rufaa kila mwaka na kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti kuu ya Taifa ya m-mama iliyoanzishwa na serikali.

Naye Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Hilda Ndambalilo  ameutaja mfumo wa M-mama kuwa ni mfumo wa usafirishaji wa dharura wa akinamama wajawazito waliojifungua ndani ya siku 42 na Watoto wachanga  wa siku 0 hadi 24.

Amesema katika mfumo huo ambao ulizinduliwa mkoani Ruvuma Mei 2023,hadi sasa umewezesha kusafirisha jumla ya wagonjwa 1,938  kati yao akinamama wajawazito 1,664 na Watoto wachanga 274.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru 2025 waikubali miradi yote Mbinga

    May 12, 2025
  • WANANCHI walivyojitokeza kuupokea mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Maguu Mbinga

    May 11, 2025
  • MAHABA ya wananchi wa Mbuji wilayani Mbinga kwa Mwenge wa Uhuru 2025

    May 11, 2025
  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.