• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI imefanya uwekezaji mkubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: October 2nd, 2024

WANANCHI wa vijiji vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,wamesisitizwa kutumia zahanati,vituo vya afya na Hospitali zinazojengwa na Serikali kwenda kufanya uchunguzi wa afya zao na kupata huduma za matibabu.

Rai  hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na Mganga Mkuu wa Halmashauri  ya Mbinga Dkt Seleman Jumbe,wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya  ikiwemo ujenzi  wa mradi  wa wodi ya wanawake,watoto na wanaume yanayojengwa katika Hospitali ya Halmashauri  iliyopo kijiji cha Kigonsera wilayani Mbinga.

Alieleza kuwa,wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanatumia vituo na Hospitali hizo kupata huduma kwa kuwa fedha zinazotumika kutekeleza miradi hiyo zinatolewa na Serikali yao na wanapaswa kujivunia  na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali.

Dkt Jumbe alisema kuwa,Serikali imetoa Sh.milioni 850 kati ya hizo Sh.milioni 500 zimepangwa kutumika kujenga wodi tatu ambazo ujenzi wake upo hatua ya kufunga milango,madirisha na kuweka malumalu na Sh.milioni 35 kwa ajili ya  kununua vifaa tiba.

“Mbali na fedha hizo Mheshimiwa Rais Samia ametupatia fedha nyingine  Sh.milioni 300 ili kujenga jengo la upasuaji,kwa sasa tupo katika hatua za manunuzi ili kumpata mzabuni kwa ajili ya kuanza ujenzi”alisema Dkt Jumbe.

Alisema,mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Halmashauri ya wilaya Mbinga ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu kwenye maeneo yao ili kuwaondolea adha ya kwenda mbali kufuata huduma za afya.

Alisema,Hospitali ya Halmashauri kwa sasa inahudumia zaidi ya wakazi 60,000, hata hivyo matarajio yao majengo mapya yatakapokamilika  idadi  ya wananchi itaongezeka kutokana na uwepo wa huduma  muhimu ikiwemo za upasuaji.

Kwa mujibu wa Dkt Jumbe,Halmashauri ya wilaya Mbinga  kuna vituo 8 vya afya,lakini mkakati uliopo kujenga vituo vingine kwa kila kata na wameanza kujenga vituo viwili katika kata ya Linda na Mkumbi ambapo ujenzi wake unaendelea vizuri.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya  Halmashauri ya wilaya Mbinga Dkt Salum Bundala,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha zilizowezesha kujenga majengo matatu ya wodi ya akina mama,wanaume,watoto na jengo la utawala ambayo yakikamilika yataondoa adha iliyopo ikiwemo ukosefu wa wodi ya kulaza wagonjwa.







Alisema, wanalazimika kutumia moja ya majengo yaliyopo kwa ajili ya kulaza wagonjwa na mama wajawazito wanatumia moja ya jengo la wagonjwa wa nje kwa ajili ya kupata huduma za  uzazi na kujifungua na wagonjwa wengine watapata wodi ambayo itasaidia kupunguza msongamano  wanapofika kupata matibabu.







Kaimu katibu wa afya  Dickson Simangwe  alitaja majengo yaliyokamilika katika Hospitali hiyo ni jengo la wagonjwa wa nje(OPD)maabara,jengo la kufulia,jengo la kutunzia dawa na vifaa tiba,kichomea taka,jengo la wagonjwa mahututi,utawala na jengo la mionzi.







Alitaja vituo vipya vinavyojengwa na gharama zake ni kituo cha afya Mkumbi(500 ml)kupitia fedha za tozo,kituo cha afya Nyoni(500ml)kutoka mapato ya ndani,kituo cha afya Linda(179ml mapato ya ndani.







Alisema,kituo cha afya Kindimbachini kinachojengwa kwa gharama ya Sh.milioni 500 fedha kutoka Serikali kuu ambapo  itahusisha  ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje,maabara,jengo pacha la huduma za uzazi,upasuaji,jengo la kufulia na kichomea taka na wamepokea Sh.milioni 90  kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi watumishi watatu(Three in one).






Alitaja vituo  vilivyokamilika na kuanza kutoa huduma ni kituo cha afya Litumbandyosi kilichojengwa kwa gharama ya Sh.milioni 598 kupitia mapato ya ndani na kituo cha afya Matiri kilichogharimu Sh.milioni 500.






Mkazi wa kijiji cha Kigonsera Rehema Mbele,ameiomba Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Mbinga kumaliza ujenzi wa majengo mapya ili waweze kupata baadhi ya huduma ikiwemo ya kulaza wagonjwa  na upasuaji ambazo hazipatikani katika Hospitali  ya wilaya.






Mkazi mwingine wa kijiji hicho Semen Ndunguru alisema,matarajio yao pindi majengo hayo yakikamilika  watapata huduma za matibabu karibu badala ya kuendelea maeneo mengine.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.