Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amesema Serikali imekusudia kumuondelea mgizo wa gharama Mkulima kwa kuleta mbolea za ruzuku
Hayo ameyasema katika mnada wa pili wa korosho uliofanyika hivi karibuni wilayani umo, wakati akizungumza na wakulima na baadhi ya wanunuzi walioshiriki mnada huo
Mtatiro amesema msimu wa 22/23 Serikali imeshatekeleza wajibu wake kwa kuwashushia wakulima bei ya mbolea kupitia mfumo wa mbolea za ruzuku lengo likiwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na ya biashara
“Mheshimiwa wetu Rais, Samia amefanya kazi kubwa sana na yakujitolea katika eneo la mazao na katika eneo la wakulima lakini nia ya Mhe Rais kwamba kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye zao la korosho pia na katika mazao mengine” amesema Mtatiro.
Hata hivyo amemshukuru Rais, Samia kwa kuweza kushusha bei ya mbolea pia amewataka na kuwasisitiza wakulima Tunduru kuweka nguvu kwenye mazao mengine ya kibiashara ili kuondokana na hasara za kushuka kwa bei ya zao na balada yake mazoa mengine yanakupa faida.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.