MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Philip Mpango amesema amekataa kupanda ndege na kuutumia usafiri wa barabara ili kuona changamoto ya barabara ya Makambako hadi Songea.
Dkt,Mpango ameeleza hayo wakati anazungumza na wananchi wa vijiji vya Lilondo na Mlilayoyo mkoani Ruvuma baada ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma..
"Watu wangu walijaribu kunishawishi niende kwa ndege nikawaambia sisi hatutawali hayo mawingu nataka kupita watu wangu waliko,kwa kweli moja ya sababu zangu za msingi ni kuona barabara hii (Makambako - Songea) bahati nzuri naibu waziri ametoa maelezo kwa hiyo ninataka kusisitiza vipande vyote ambavyo vimewekewa fedha kwenye bajeti ya mwaka huu muanze kufanya kazi mara moja.
Dkt Mpango amesema serikali imetenga fedha kuanza kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami nzito kipande cha Songea hadi Lutukila chenye urefu wa KM 98 na kwamba utekelezaji wa mradi huo unaanza mwaka huu.
Dkt,Mpango ameagiza wizara ya Fedha kuhakikisha inatafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kutoka kipande cha kutoka Lutukila kufika Makambako kwa kuwa chakula kingi kinatoka mikoa ya kusini hasa mkoa wa Ruvuma ambao ni kapu la chakula nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango ameanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma inayotarajia kukamilika Julai 24,2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.