SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza zoezi la kuratibu madai na madeni ya watumishi yote yasiyokuwa ya mishahara kwa njia ya kieletroniki.
Muwezeshaji wa Mafunzo ya mfumo wa madeni (MADENI MIS) kutoka Wizara ya TAMISEMI Nestory Mgimwa akitoa mafunzo kwa wakuu wa Idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea,amesema kundi la kwanza kunufaika na mfumo huo ni walimu.
Mgimwa amesema Serikali imeanza kuratibu madeni hayo kwa lengo la kuyatambua na kuyaingiza kwenye mfumo wa MADENI MIS ili kupata takwimu sahihi za madeni halali ya watumishi na kukabiliana na udanganyifu wa madeni hewa.
Amezitaja faida za mfumo huo kuwa ni kuongeza uwazi, uwajibikaji, ari ya kufanya kazi na kuondoa usumbufu na gharama kwa watumishi wakati wanafuatilia stahiki za madeni yao.
“Wanufaika wa kwanza kwenye mfumo huu ni walimu ambao ni asilimia 52 kati ya watumishi wote wa Halmashauri nchini”, amesema Mgimwa.
Hata hivyo amesema,watumishi katika mfumo huu wanatakiwa kutoa taarifa za ukweli na sahihi katika kudai madai yao kwa kuleta viambatanisho stahiki na kwamba ni kosa la kisheria kugushi nyaraka kwa lengo la kujipatia malipo.
Zoezi la kuratibu madai na madeni ya walimu limeanza Agosti 3 mwaka huu na linatarajia kukamilika Agosti 18,2020 katika mikoa yote nchini.
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Septemba 8,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.