Waziri wa Ujenzi, Mhehshimiwa Innocent Bashungwa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho ya kusaini i mkataba na kumtangaza Mkandarasi atayejenga barabara ya Likuyufusi - Mkenda (km 122) wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika daraja la Mkenda lililopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji Waziri wa Ujenzi amesema mkataba unatarajia kusainiwa hivi karibu kwa ajili ya ujenzi sehemu ya kwanza barabara kuanzia Likuyufusi - hadi Mkayukayu kilometa 60 kwa kiwango cha lami.
Amesema .Ujenzi wa barabara hiyo utaenda sanjari na ujenzi wa Daraja la Kisasa la Zege lenye urefu wa Meta 144 mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji eneo la Mkenda Wilayani Songea hivyo kuufungua Mkoa wa Ruvuma kiuchumi.
Amesema darala lililopo hivi sasa lenye urefu wa meta 98 litabomolewa na kuwekwa daraja la kisasa lenye uwezo wa kubeba magari makubwa na kupishana kwenye daraja ambalo litakuwa na njia mbili
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.