• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI kujenga kituo cha wanyamapori Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: August 21st, 2022

SERIKALI kupitia mamlaka ya usimamizi wanyapori Tanzania(Tawa) kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya Tunduru,imeanza kujenga kituo kikubwa  cha  askari wa wanyamapori ili kudhibiti wanyama wakali na waharibifu wanaovamia makazi ya watu na kuharibu mazao mashambani.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira wilaya ya Tunduru Ombeni Hingi,kwa mkuu wa wilaya  hiyo Julius Mtatiro aliyetembelea ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa  katika kijiji cha Chingulungulu kata ya Muhuwesi.

Hingi alisema,lengo la kujenga kituo  hicho ni katika jitihada za Serikali  za kudhibiti na kukabiliana na changamoto kubwa  ya wanyama  hao hasa Tembo  wanaotoka porini na kwenda kwenye makazi ya watu.

Alisema,wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa maeneo yenye changamoto kubwa ya wanyama wanaohatarisha maisha ya watu na kuharibu mashamba,hivyo Serikali imeona ni vyema kujenga kituo hicho ambacho kitakuwa na askari watakaofanya kazi ya kudhibiti wanyama hao.

Kwa mujibu wa Hingi,walifanya jitihada mbalimbali kuomba msaada katika taasisi,idara za Serikali na  zisizo za Serikali ili kuwasaidia kukabiliana na wanyama hao,lakini wizara ya maliasili na utalii kupitia Tawa ndiyo waliokubali kutoa  Sh.milioni 80 kwa ajili ya kujenga kituo hicho.

Alisema,kwa sasa  Halmashauri ya wilaya  Tunduru kupitia idara ya  maliasili inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendea  kazi na watumishi ambao wako tisa(9) tu hivyo ,hawawezi kutokana na tatizo kubwa la wanyama  hao katika wilaya ya Tunduru.

Alisema,kujengwa kwa kituo hicho na vituo vingine vidogo vitakavyojengwa hapo baadaye ambavyo vitakuwa na askari wengi kutaongeza nguvu katika jitihada za kukabiliana na wanyamapori.

Kwa upande wake Afisa Wanyamapori wa wilaya  hiyo Limbega Hassan alisema,kijiji cha Chingulungulu na kata ya Muhesi ni maeneo yenye changamoto kubwa ya kuvamiwa na wanyamapori mara kwa mara.

Alisema,kujengwa kwa kituo hicho katika kijiji hicho ni kama bahati kwani kuna maeneo mengi yenye uhitaji wa askari wa wanyamapori  na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa askari watakaoletwa ili waweze kutekeleza majukumu yao  badala ya kuwaogopa.

Diwani wa kata ya Muhuwesi Imani Ngonyani amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali  kwa fundi aliyepewa kazi ya kujenga kituo hicho na hata kwa askari watakaoletwa kwa ajili ya kusaidia wananchi kukabiliana na wanyama hao.

Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa usikivu wake na kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Tunduru  katika kudhibiti matukio ya kushambuliwa na Tembo.Alisema,tatizo la wananchi kushambuliwa na tembo katika maeneo yao limekuwa kubwa kutokana na wilaya hiyo kwa sehemu kubwa kuzungukwa na Hifadhi ya Nyerere yenye wanyama wengi wakali na waharibifu wa mazao.

Ameitaka idara ya maliasili wilaya,kuendelea kuomba na kutafuta fedha kwa wahisani mbalimbali ambao watasaidia kuendelea kujengwa kwa vituo vingine katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kwa ajili ya makazi na ofisi za askari wa wanyamapori.

Alisema, kituo hicho ni mwanzo tu na kuhaidi kuwa serikali ya wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kujenga vituo vingi  vya askari ili kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.

“nimekaa Tunduru miaka mitatu sasa natambua ukubwa  wa tatizo la Tembo,hatuwezi kuwaacha wananchi wanaendelea kufa na mazao yao yanaliwa, sisi kama viongozi tuliopewa dhamana ni lazima tuanze kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi wetu bila kutegemea serikali kuu”alisema Mtatiro.

Amemwagiza fundi kuhakikisha anawatumia vijana wanaotoka katika eneo hilo katika ujenzi wa kituo hicho,badala ya kuwatumia vijana kutoka nje ya kata hiyo  na kuwashukuru viongozi wa vijiji na kata kwa uamuzi wa kutoa ardhi bure.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.