SERIKALI inatarajia kujenga maghala 11 ya kuhifadhia nafaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama katika ziara ya kikazi katika Kata ya Magagura ambapo amesema Kati ya Maghala ya chakula 28 yatakayojengwa Mkoani Ruvuma, Maghala 11 yatajengwa Halmashauri ya wilaya ya Songea,
Akitoa ufafanuzi kwa wandishi wa habari Mkandarasi wa jengo hilo Eng. Julius Nalitolela alisema “ hili ni ghala hapa Masangu, ni kati ya maghala kumi na moja yanayojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Songea, pia kati ya maghala 28 yaliyopo Mkoa wa Ruvuma. Mradi huu unaghalimu kiasi cha shilingi Milioni mia tano ishirini ( 520,000,000.00) ni Mradi ambao utaweza kuhifadhi vyakula mbalimbali kiasi cha Tani elfu moja ( 1000) na litakua na ukubwa wa Squre meter mia tano sitini ( 560) ambalo pia itakua na ofisi na vyoo kwa ajili watumishi.
Akikagua Ghala hilo Mhe. Jenista aliwataka viongozi na wasimamizi kuwapatia nafasi wazawa katika kazi ndogondogo za pale ili waweze kujipatia kipato, pia akashauri hata kandarasi ndogo ndogo ziweze kupewa kwa wazawa ili kukuza uchumi wa kijiji cha Masangu.
“ kwanza niwapongeze Halimashauri kwa kusimamia vema miradi ya serikali, nikupongeze Mkurugenzi Neema Maghembe na timu yako nzima, lakini nishauri pia vipaumbele vya ajira viwe kwa wazawa, ili waweze kujipatia kipato kutokana na vitu vinavyofanyika kwenye maeneo yao ikiwemo pia kupewa kandarasi ndogo ndogo wazawa wa hapa hapa kijijini. Natoa wito pia kwa wanakijiji kuwa walinzi wa mali za Serikali"
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.