• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI kutumia ziwa Nyasa kupunguza kero ya maji nchini

Imewekwa kuanzia tarehe: November 11th, 2022

MKURUGENZI Mkuu wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)Mhandisi Clement Kivegilo amesema,kuna haja ya Serikali kuanza mchakato wa kutumia maji ya ziwa Nyasa ili kumaliza  shida ya maji  kwa wananchi,badala ya kuendelea kutegemea vyanzo vya maji ambavyo sio vya uhakika.

Kivegilo amesema hayo  kwa nyakati tofauti,wakati akikagua ujenzi wa miradi mikubwa ya maji katika kata ya Liuli na Lituhi Halmashauri ya wilaya Nyasa mkoani Ruvuma inayojengwa kwa gharama ya Sh.bilioni 11.3

Kivegilo alisema,hakuna sababu ya wilaya ya Nyasa kuwa na tatizo la maji kwa wananchi wake,kwani kuna vyanzo vingi na uhakika ikiwamo ziwa Nyasa lenye uwezo wa kuhudumia wilaya yote ya Nyasa.

“unaposikia watu wana shida ya maji  na wanaishi kando ya ziwa nyasa haiingii akilini hata kidogo,wakati umefika sasa kwa serikali kuanza mchakato wa kutumia maji ya ziwa Nyasa badala ya kuendelea kutegemea vyanzo vingine ambavyo havina uhakika sana”alisema Kivegilo.

Miradi hiyo ni mradi  wa maji Liuli unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 5 na mradi wa maji wa Mwerampya kata ya Lituhi unaotekelezwa kwa gharama ya  zaidi ya Sh.bilioni 6.5.

Amemwagiza Mkandarasi kampuni ya Emirate  Co Ltd anayejenga miradi hiyo,kuhakikisha anakamilisha kazi kabla ya muda aliopewa ili wananchi waanze kupata huduma ya maji katika maeneo yao.

Amamtaka kukamilisha ujenzi wa vituo vya kuchotea maji,ili huduma ya maji ianze kufika kwa wananchi huku kazi nyingine zikiendelea kufanyika kwani hakuna sababu ya wananchi kutopata maji kama mradi umefikia asilimia zaidi ya 65 ya utekelezaji wake.

Kwa mujibu wa Kivegilo ni kwamba,miradi yote ni ya mserereko hivyo hakuna changamoto kubwa katika utekelezaji wake, kwa hiyo ni vyema mkandarasi akaongeza  nguvu ili ikamilike haraka na  kuanza kutoa huduma  na wananchi wa vijiji hivyo wafurahie matunda ya Serikali yao ya awamu ya sita.

Alisema kwa sasa kazi zilizobaki siyo kubwa, hivyo mkandarasi ana uwezo wa kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kabla ya muda aliopewa kwa sababu kampuni hiyo ina uwezo mkubwa katika kujenga miradi ya maji hapa nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya ya Nyasa Jeremiha Maduhu alisema,miradi hiyo yote inatarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2023 na itawanufaisha zaidi ya wakazi  28,000.

Naye Mbunge wa jimbo la Nyasa Stella Manyanya,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha  zaidi ya Sh.bilioni 11 ambazo zinakwenda kutumika kujenga miradi miwili mikubwa ambayo itamaliza tatizo la muda mrefu  la huduma ya maji safi na salama.

Hata hivyo,ameiomba wizara ya maji kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga miradi mingine ya maji katika vijiji vyenye changamoto kubwa ya huduma hiyo.

Mkazi wa Nyasa  Said Rashid alisema,kwa muda  baadhi ya maeneo ya Jimbo la Nyasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya maji katika maeneo yao.

Alisema,kujengwa kwa miradi hiyo kutapunguza kero hiyo hasa kwa wanawake na watoto wanaolazimika kuamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji kwevye vyanzo vichache  vilivyopo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.