Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaweka mikakati ya kuzuia UKIMWI pamoja na kupunguza changamoto ya Afya ya akili kwa Watumishi Umma nchini
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Leila Mavika katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 23-24 cha kudhibiti maambukizi ya VVU,UKIMWI na Magonjwa ya sugu yasiyoambikizwa (MSY) kilichofanyika Mkoani Ruvuma.
Amesema Serikali inatambua Watumishi wa Umma kama sehemu ya Jamii ambayo ni miongoni mwa wahanga wa Magonjwa hayo ambapo yamesababisha kushusha kasi ya ufanisi na utendaji kazi hivyo kuwalazimu kutumia muda mwingi kupata matibabu na kufuatilia huduma za Afya.
“Serikali Kwa kutambua umuhimu wa Afya na Ustawi wa Watumishi wa Umma nchini, iliandaa muongozo wa waraka namba mbili wa mwaka 2014, kuhusu udhibiti wa VVU,UKIMWI na Magonjwa ya sugu yasiyoambikizwa mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma”amesema Mavika
Mavika ameeleza kuwa lengo kuu la Serikali ni kuwajengea uelewa Watumishi wote wa Umma kuhusu muongozo wa waraka ili kupunguza hali ya unyanyapaa na kuhamasisha Watumishi kujiweka wazi kulingana na hali walizo kuwa nazo
Aidha, amatoa magizo kwa Mamlaka za ajira nchini kutenga fedha za muongozo na waraka ili kuwezesha utekelezaji wa mpango huo pamoja na kutenga muda wakufanya mazoezi ya pamoja kwa Watumishi walau mara moja kwa Mwezi
Naye kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Gilbert Simya amesema kuwa maagizo yote pamoja na maelekezo yatafanyiwa kazi kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya Halmashauri ili kuhakikisha Serikali inakuwa na nguvu kazi yenye tija
“Naishukuru Serikali kwa kuhakikisha inawezesha na kujali mazingira ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Ruvuma ambao wanapitia changamoto ya magonjwa yasiyoambukizwa pamoja na UKIMWI kwa kukutoa posho ya uhimarishaji wa afya zao”amesema Simya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.