• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI kuwalipa wananchi 900 bilioni 5.3 fidia ya ardhi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: August 13th, 2023

SERIKALI ya Awamu ya Sita imetenga shilingi bilioni 5.3 ili kuanza kuwalipa wananchi 900 fidia ya ardhi ya eneo la  Export Processing Zone Authority (EPZA) lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 5000 katika kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa EPZA Charles Itembe kwenye  Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo uliofanyika hivi karibuni kwa lengo la kufanya uhakiki wa wananchi watakaonufaika  na fidia hiyo ili waanze kulipwa.

Mkurugenzi huyo wa EPZA amewahakikishia wananchi hao kuwa madai yao  yamefikia hatua ya ukamilishaji wa malipo ili wananchi waanze kulipwa na serikali ianze kuliendeleza eneo hilo baada ya wananchi wote kulipwa fidia.

Hata hivyo Itembe alisema malipo hayo kwa mara ya kwanza yalilipwa kwa baadhi ya wananchi na awamu ya pili yatatolewa kwa wananchi ambao hawakulipwa.

 Amesisitiza kuwa  kabla ya kuanza kulipwa utafanyika uhakiki wa majina katika ofisi ya kata Mwengemshindo ambapo wanufaika watahakikiwa kwa kuleta viambatanisho vikiwemo  kitambulisho, picha, pamoja na barua kutoka Serikali ya Mitaa ili malipo yalipwe kwa mtu anayestahili na kwamba malipo yote yatalipwa kwa kupitia Akaunti za benki.

Mkurugenzi huyo wa EPZA amesema Serikali baada ya kukamilisha malipo hayo na kupewa hatimiliki ya eneo hilo itaanza uwekezaji kiuchumi hivyo kuchochea uchumi wa mji wa Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Naye katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba akizungumza kwenye mkutano huo amewataka wananchi wa Kata ya MwengeMshindo kujitokeza kwenye zoezi la Uhakiki ili kuondoa malalamiko yanayoweza kuathiri zoezi hilo.

 “EPZA wamekuja kulipa fidia ya viwanja na kila mwananchi mnufaika wa fidia hizi atalipwa kulingana na ukubwa wa eneo lake, na kila mnufaika atalipwa fidia kulingana na uthamini uliofanyika bila udanganyifu wowote’’,alisisitiza.

Kwa upande wake Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alex Mshana aliitaja kero kubwa ya wananchi wa Mwengemshindo ilikuwa ni madai ya fidia ya ardhi eneo la EPZA Mwengemshindo ambapo sasa serikali imetoa fedha za kuwalipa.

Amesema  mara baada ya malipo ya fidia hiyo wananchi watatakiwa kupisha maeneo hayo ili  yaendelezwe na uwekezaji wa matumizi ya umma kupitia EPZA uweze kufanyika.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi,Diwani wa Kata ya Mwengemshindo Mheshimiwa Osmond Kapinga  ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za fidia kwa wananchi hao hivyo kumaliza kero hiyo ya muda mrefu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.