Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali, Ahmed Abbas Ahmed,amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada kubwa za kuendeleza sekta ya Kilimo
Ametoa pongezi hizo katika uzinduzi wa Minada ya Zao la korosho katika Mkoa wa Ruvuma, ambao ulifanyika Oktoba 22, 2024 katika Kata ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru.
Kanali Abbas ameitaja moja ya Changamoto kubwa iliyokuwa inakabili wakulima ni ucheleshwaji wa malipo kwa wakulima jambo ambalo kwa msimu huu limedhibitiwa kwa malipo hayo kufanyika kupitia kituo kimoja cha Malipo
Kanali Abbas ametoa rai kwa wakulima kuendelea kujifunza kuongeza thamani ya zao la Korosho , kwa kuanzisha viwanda vya ubanguaji wa korosho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU LTD), Ndg. Mussa Manjaule, amesema Serikali imefanya jitihada za kuhakikisha wakulima wa zao la korosho wanapata bei nzuri, pia imehakikisha inaleta viuatilifu kwa wakati ili kuweza kuongeza iuzalishaji wa zao hilo.
Sanjali na hilo, Manjaule ametoa wito kwa Wakulima kuzingatia kanuni na taratibu bora za uvunaji na utunzaji wa zao la korosho ili ziweze kuwa na thamani sokoni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.