HATIMAYE serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imesikiliza kilio cha wananchi wa Mkili wilayani Nyasa mkoani Ruvuma baada ya kutoa shilingi bilioni 3.199 za kujenga daraja la Mkili lenye urefu wa mita 20 na njia zake za maingilio kupitia Mkandaarsi Ovans Construction ambapo sasa wananchi wataweza kuvuka eneo la mto wakati wote.
Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameishukuru serikali kwa kuanza mradi wa ujenzi huo ambapo amesema watu wengi walikuwa wanapoteza maisha kila mwaka wakati wanavuka Mto huo kipindi cha mvua za masika na hata wanafunzi waliathirika kimasomo kwa kuwa mvua zinaponyesha watoto walikuwa hawaendi shuleni
Pichani ni eneo la mto ambako daraja hilo linajengwa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.