Wananchi wa vijiji vya Mkenda na Nakawale katika Halmashauri ya Songea Vijijini pamoja na wananchi wa kijiji cha Mitomoni, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja la Mto Ruvuma lenye urefu wa mita 45 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 8.8.
Msimamizi MKuu wa mradi huo kutoka TANROADS, Mhandisi Fedinandi Mdoe, amesema ujenzi wa daraja hilo tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 3 mwaka huu, ambapo gharama ya mradi ni Shilingi bilioni 9.293.
Alibainisha kuwa utekelezaji wa mradi huo ulianza rasmi Novemba 7 mwaka jana.
Kwa upande wake, Mhandisi Blanka Mkundelinda, mkaguzi wa vifaa vya ujenzi katika mradi huo, amesema kuwa vifaa vingi vya ujenzi tayari vimepatikana, ambapo baadhi vimepelekwa kwenye maabara za Songea na Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo, na vingine tayari vimefikishwa eneo la mradi lililoanza kujengwa.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Salehe Juma, amesema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya kizalendo ya Ovans kutoka Wilaya ya Mbinga, na kazi inaendelea vizuri.
Ametoa rai kwa wananchi wa maeneo husika kulinda miundombinu hiyo ili isihujumiwe baada ya kukamilika, kwani inajengwa kwa gharama kubwa.
Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mfuko wa dharura, na wafadhili hao wanataka mradi ukamilike kwa wakati bila kuchelewa, kwani fedha zote za utekelezaji tayari zimeshatolewa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.