SERIKALI imetatua kero ya umeme katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma baada ya kufikisha huduma ya umeme katika vijiji 81 kati ya vijiji 84 vilivyopo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri amesema katika Wilaya ya Nyasa vimebakia vijiji vitatu ambavyo bado havina umeme ambavyo Mkandarasi yuko kazini anaendelea na kazi ya kupelaka Umeme katika vijiji hivyo.
Magiri ameyasema hayo wakati anazungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndengere Kata ya Mbamba bay Wilayani Nyasa.
Amewataka wananchi ambao hawajapata huduma ya umeme kuwa wavumilivu kwa kuwa nia ya Serikali ni kufikisha umeme katika ngazi ya kila kijiji na awamu itakayofuata ni kufikisha umeme katika ngazi ya Kitongoji.
“Serikali yetu ni Sikivi kama imeweza kupeleka umeme katika Vijiji 81 katika Wilaya ya Nyasa haitashindwa kufikisha umeme katika Vitongoji’’,alisisitiza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.