Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma ni mojawapo ya hospitali kongwe nchini Tanzania iliyojengwa mwaka 1930.
Hospitali hii imefanyiwa ukarabati mkubwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya majengo ya hospitali hiyo pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.
Ukarabati huu unahusisha majengo muhimu kama vile jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, na jengo la upasuaji.
Kwa ujumla, juhudi hizi za ukarabati na uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru zinaonesha dhamira ya serikali katika kuboresha sekta ya afya .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.