Serikali Wilayani Nyasa, kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania, Imekabidhi Vitabu 712 vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni thelathini, katika Shule ya Sekondari Mbamba bay, ili kutatua changamoto ya upungufu wa Vitabu vya masomo mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba Amekabidhi vitabu hivyo jana katika Ukumbi wa Kassim Majaliwa Uliopo katika Shule ya Sekondari Mbamba Bay, Wilayani hapa, na kumpongeza Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Mwl Rogers Semwalekwa kwa kufanya Ufuatiliaji katika Shule zote za Sekondari Wilayani Hapa, na Kubaini changamoto mbalimbali zilizopo katika shule, na kizipatia ufumbuzi kwa haraka.
Mh. Chilumba ameongeza kuwa mwl Semwalekwa ni mfano wa kuigwa na walimu, wafanyakazi wengine, Wakuu wa Idara zingine kwa kuwa amekuwa mbunifu wa kuzifuatilia shule zake, kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa haraka kwa kutumia ubunifu wake wa kwenda Taasisi ya Elimu Tanzania, na kupatiwa Vitabu Hivyo.
Aidha ametoa wito kwa wakuu wa Idara na vitengo Wilayani hapa, kuwa wabunifu na kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kuyapatia ufumbuzi.
Awali Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbamba Bay Mwl Zawadi Msambwa akitoa Taarifa Fupi Kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, amesema kupatikana kwa vitabu hivyo kutawaongezea wanafunzi ari ya kujifunza kwa kuwa awali kulikuwa na Upungufu wa Vitabu hasa vya kidato cha Tano na Sita, kwa hiyo wanaishukuru Taasisi ya Elimu Tanzania na Afisa elimu Sekondari Nyasa kwa Juhudi zake za kutatua Changamoto katika Shule zake.
Aidha amevitaja vitabu alivyopokea kuwa ni Vitabu vya Chemistry,Biology,Kiswahili, na Mathematics.
Naye afisa Elimu Sekondari Wilayani hapa amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani, na kuahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali katika shule zote Wilayani Nyasa ili waweze kupata elibu bora.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw. Eiphrem Kawonga amempongeza kwa Dhati Afisa Elimu Huyo na kumtaka aendelee na juhudi hizo za kutatua changamoto zinazoikabili Idara ya Elimu Sekondari Kama alivyofanya.
Kwa upande wao, Wanafunzi wa Sekondari Mbamba bay Wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kwa kutatua changamoto Mbalimbali katika shule yao na kuahidi kusoma kwa bidii na kuitangaza vema Shule hiyo kwa kutoa Elimu bora na Kuwaandaa wanafunzi katika Soko la ushindani wa Elimu na Ajira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.