Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo kidato cha sita huku watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa 84,212 waliofanya mtihani kidato cha sita Juni/Julai 2020 wamefaulu.Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde amesema, watahiniwa 85,499 walisajiliwa kufanya mtihani huo.Amesema, kati yao wasichana walikuwa 36,168 sawa na asilimia 42.30 na wavulana walikuwa 49,331 sawa na asilimia 57.70.Dk. Msonde amesema, kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 74,753 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 10,746.Amesema, kati ya watahiniwa 85,499 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 84,212 sawa na asilimia 98.49 walifanya mtihani na 1,287 sawa na asilimia 1.51 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ugonjwa na utoro.Katibu mtendaji huyo amesema, watahiniwa wa shule, kati ya 74,753 waliosajiliwa, watahiniwa 74,284 sawa na asilimia 99.37 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 32,403 sawa na asilimia 99.60 na wavulana 41,881 sawa na asilimia 99.19.Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea, Dk. Msonde amesema, watahiniwa 10,746 walisajiliwa, watahiniwa 9,928 sawa na asilimia 92.39 walifanya mtihani na 818 sawa na asilimia 7.61 hawakufanya mtihani.Jumla ya watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita wamefaulu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.