MKOA wa Ruvuma umepokea shilingi bilioni 12.7 sawa na asilimia 2.4 ya shilingi bilioni 635.68 ambazo zimeidhinishwa na TAMISEMI kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya Afya,Elimu na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika kikao kazi cha maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ,kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea
“Matumizi ya fedha hizi yameelekezwa kwenye maeneo ya vipaumbele yanayogusa wananchi moja kwa moja ili kuwaondolea kero katika na kupata huduma za afya,elimu na uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuwakinga dhidi ya UVIKO 19”’alisisitza RC Ibuge
Akifafanua kuhusu fedha hizo Brigedia Jenerali Ibuge amesema sekta ya elimu imetengewa shilingi bilioni 10.32 kati ya fedha hizo elimu msingi imetengewa bilioni 1.36 kwa ajili ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa na elimu sekondari imetengewa bilioni 8.96 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 448 vya madarasa kwa ajili ya kujiandaa kupokea wanafunzi wa wa kidato cha kwanza Januari 2022.
Kwa upande wa sekta ya afya Brigedia Jenerali Ibuge amesema jumla ya shilingi bilioni 2.38 zimetengwa kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa huduma za dharura ,kujenga jengo la wagonjwa mahututi na kununua mitambo miwili ya huduma za mionzi.
Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote kusimamia ujenzi wa madarasa ya sekondari na kwamba ifikapo Desemba 30,2021 pasiwepo na upungufu tena wa vyumba vya madarasa na kusisitiza kuwa Halmashauri ambayo itakuwa na upungufu itumie vyanzo vya mapato ya ndani kujenga madarasa Hayo .
RC Ibuge amewaagiza watendaji kwenye Halmashauri zote kuhakikisha kuwa wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo kuwashirikisha wananchi tangu hatua za awali za utambulisho wa miradi.
katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO 19,zilizowezesha nchi kupata mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwa ajili ya kampeni Maendeleo ya uchumi na mapambano ya UVIKO 19.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 20,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.