SERIKALI imetoa shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika shule za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Rashid Bundala amesema fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2023/2024.
Amebainisha kuwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo imetumia Shilingi Milioni 184 kutekeleza ujenzi wa matundu 8 ya vyoo katika shule ya sekondari Namswea, ujenzi wa matundu ya vyoo 12 katika shule ya Sekondari Mkumbi pamoja na ujenzi wa matundu 6 ya vyoo katika shule ya Sekondari Luhagara.
Bundala ameeleza kuwa Serikali kupitia mradi wa Secondary Education Quality Improvement Programme (SEQIP) imetoa shilingi bilioni 1.1 kutekeleza ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kitumbalomo, ujenzi wa bweni shule ya sekondari Hagati,ukamilishaji wa vyumba Vitatu vya madarasa shule ya sekondari Hilela, ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Kipapa na ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Mndeme.
Aidha amebainisha kuwa Serikali kupitia mradi wa Education perfomance for results ( EP4R) imetoa kiasi cha shilingi milioni 176 kutekeleza ujenzi wa bweni moja na utengenezaji wa vitanda 40( double decker) katika shule ya Sekondari Ruanda pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Ruanda
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.