WAKALA wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Ruvuma,umepokea Sh.bilioni 2.5 kati ya Sh.bilioni 6 ilizoomba ili kurejesha miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua za masika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Saleh Juma,baada ya kukagua kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya daraja la Mto maarufu la Namiungo wilayani Tunduru.
Saleh,amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwa kuidhinisha fedha hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwenye maeneo yenye changamoto ili kutoa fursa kwa shughuli za usafiri na usafirishaji kuendelea kama kawaida.
Amesema,licha ya mvua za masika kunyesha kwa wingi katika Mkoa Ruvuma,barabara zote zilizo chini ya TANROADS zinapitika na hakuna shughuli za kijamii zilizosimama kutokana na ubovu wa barabara.
Mwezi Machi mwaka huu daraja la Namiungo lilipata athari kubwa baada ya maji ya mvua kupita juu ya daraja na kuharibu miundombinu,hali iliyosababisha magari kupita upande mmoja.
Meneja huyo wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma amesema,kazi ya kurejesha miundombinu ya daraja hilo imechelewa kukamilika kutokana na changamoto ya mvua, ambapo magari ya mkandarasi yameshindwa kufika maeneo yanakopatikana mawe na vifusi.
Hata hivyo,amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi mwishoni mwa mwezi huu ili barabara hiyo irudi kwenye hali yake na wananchi waendelee kuitumia katika shughuli zao za uzalishaji mali.
Mhandisi wa kampuni ya Ovans Constructions Ltd iliyopewa kazi ya matengenezo ya daraja la Namiungo Azimio Mwapongo amesema,amehaidi kufanya kazi usiku na mchana ili waweze kukamilisha kazi mwisho wa mwezi huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.