Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi biioni 7.2 kujenga shule mpya za msingi 12 mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema fedha hizo zimetolewa na serikali kupitia program ya uboreshaji wa shule za msingi na awali (BOOST) kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi 12, na ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule za msingi 44.
Amebainisha kuwa kati ya fedha hizo Zaidi ya shilingi bilioni 4.3 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ambao unahusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya msingi 98, vyumba vya madarasa ya Elimu ya Awali ya mfano 24, matundu ya vyoo ya msingi 136, matundu ya vyoo ya Elimu ya Awali 72, matundu ya vyoo vya walimu 24, vichomea taka 12 na majengo ya utawala 12.
Kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Zaidi ya shilingi bilioni 2.9 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambayo inahusisha vyumba vya madarasa ya msingi 87, matundu ya vyoo msingi 114, vyumba vya madarasa ya elimu ya awali ya mfano 16, matundu ya vyoo Elimu ya Awali 48, na nyumba za walimu mbili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.