Wanafunzi 49 wenye ulemavu wa shule ya Msingi na ufundi Namtumbo Mkoani Ruvuma watanufaika na na mradi wa bweni ambalo serikali imetoa shilingi milioni 100 Kwa ajili ya wanafunzi wa kitengo Cha elimu maalumu Shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi na ufundi Namtumbo Mustapha Ponera amesema shule yake ilipewa fedha milioni 100 kutoka Lanes II Kwa ajili ya kujenga bweni la watoto wenye mahitaji maalumu Shuleni hapo
Hata hivyo Ponera amesema ujenzi wa bweni Hilo lipo katika hatua za umaliziaji na mara ujenzi huo utakapo kamilika wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu wataanza kulala katika bweni Hilo.
Kitengo Cha elimu maalumu katika shule ya msingi na ufundi Namtumbo kina jumla ya walimu 4 kukiwa na walimu wa like 2 na wakiume 2 huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 49 wanafunzi wavulana 33 na wanafunzi wa kike 16 .
Shule ya msingi na ufundi Namtumbo IPO katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo Ina jumla ya wanafunzi 845 ambapo kati ya wanafunzi hao , wanafunzi 49 ni wanafunzi wa kitengo Cha elimu maalumu ambao wamejengewa bweni Hilo waweze kulala shuleni hapo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.