KAMATI ya Fedha Halmashauri ya Madaba wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Igawisenga iliyoghalimu kiasi cha shilingi Milioni 50 kutoka Serikali kuu.
Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igawisenga George Karata akisoma taarifa kwa Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa amesema ujenzi ulianza Januari 2,2023 kwa kutekelezwa kwa force account.
Karata amesema hadi kufikia sasa ujenzi umefikia hatua ya kupaua,kuezeka,blandaring,kufunga dari na skimming ya dari.
Amesema zaidi ya shilingi milioni 43 kimetumika kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya viwandani na visivyo vya viwandani pamoja na malipo ya mafundi na ujenzi huo unatarajia kukamilika Juni 30,2023.
Hata hivyo ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwalimu,na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama pamoja na Diwani wa Kata ya Wino ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa kwa jitihada wananzofanya kuhakikisha wanapata miradi ya Maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.