MILIONI 470 ZINAVYOTEKELEZA UJENZI SEKONDARI YA KIZUKA SONGEA
Menejimenti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imeanza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Songea.
Moja ya miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa sekondari mpya ya Kizuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 85.
Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 470 kujenga Majengo ya Utawala,madarasa manane maabara tatu,jengo la maktaba na TEHAMA.
Shule hiyo inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Mwakani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.