• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa milioni 500 kuboresha kituo cha afya Muhukuru Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: July 11th, 2020

SERIKALI ya Awamu ya Tano imetoa jumla ya shilingi milioni 500 kuboresha kituo cha afya Muhukuru kilichopo wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa uboreshaji wa kituo hicho Mganga Mfawidhi wa kituo  Dr.Denis Mhagama amesema fedha hizo zilipokelewa katika mwaka wa serikali 2017/2018 na kwamba kazi  ya ujenzi ilikamilika Machi mwaka huu.

Ameyataja majengo ambayo yamekamilika kuwa ni jengo la upasuaji,maabara,jengo la kuhifadhia maiti,nyumba ya mtumishi na wodi ya mama na mtoto.

Dr.Mhagama amezitaja huduma zinazotolewa katika kituo hicho kuwa ni matibabu ya wagonjwa wa nje,matatibu ya wagonjwa wa ndani,huduma ya mama na mtoto,upimaji wa VVU na ushauri nasaha.

Amezitaja huduma nyingine kuwa  ni kliniki ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi  vya UKIMWI,uchunguzi wa viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama,matibabu ya kifua kikuu na ukoma na huduma za upasuaji hasa kwa akinamama wenye uzazi pingamizi.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama ameishukuru serikali  na Ubalozi wa Japan kwa kutoa fedha za kuboresha kituo cha  afya Muhukuru.

Amesema kituo hicho kinahudumia kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambazo ni Lilahi,Muhukuru na Ndongosi na kwamba  kituo hicho pia kinatoa huduma kwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Nyasa na nchi jirani ya Msumbiji.

“Kukamilika kwa majengo haya kumewezesha kuokoa kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga,ambavyo vingeweza kutokea kutokana na umbali wa kituo na hospitali ya Mkoa’’,alisema.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Songea Simon Bulenganija amesema katika uboreshaji wa kituo hicho Halmashauri imechangia sh.milioni 28.2 na kwamba upatikanaji wa dawa na vitendanishi katika kituo ni zaidi ya asilimia 90 kwa walengwa wapatao 20,620.

Kituo cha Afya Muhukuru kipo umbali wa kilometa 80 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Songea,kikiwa na watumishi 25 wa kada mbalimbali.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 10,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.