Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi milioni 560.5 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya katika Kata ya Hanga, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Fedha hizo zinatumiwa kujenga madarasa manane, jengo la utawala, maabara za sayansi, maktaba, jengo la kompyuta, pamoja na vyoo vya wasichana na wavulana. Kwa sasa, shughuli za awali za ujenzi zinaendelea, zikiwemo upangaji wa mawe kwenye misingi, ujazaji wa kifusi, na ujenzi wa msingi wa maktaba na chumba cha kompyuta.
Wananchi wa Hanga wamepokea hatua hii kwa furaha, wakimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza mahitaji yao. Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya kusomea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.